Haki za Vyama vya Wafanyakazi

This page was last updated on: 2021-01-25

Uhuru wa Kujiunga na chama cha wafanyakazi / waajiri

Kulingana na kifungu cha 20 cha Katiba, kila mtu ana haki ya uhuru, kulingana chaguo huru la mtu kukutana kwa amani, kuhusika na kushirikiana na watu wengine, na muhimu zaidi kuanzisha au kujiunga na mashirika au vyama vilivyoundwa kwa ajili ya mashirika ya haki za wanadamu za wafanyakazi au mashirika mengine kwa faida yao na ambayo yameanzishwa kulingana na sheria za nchi.

Kila mtu anaweza kulinda haki na maslahi yake kupitia hatua ya chama na anaweza kujiunga na chama anachokitaka. Mfanyakazi ako huru kujiunga na chama cha wafanyakazi anachokitaka. Sheria inapiga marufuku ubaguzi wa vyama. Sheria inapiga marufufuku uundaji wa chama cha wafanyakazi kwa majaji na maafisa wote wa mahakama; wanachama wa Idara Maalum; na wafanyakazi wa Bunge.

Mwajiri hastahili kuhitaji mfanyakazi kujiunga au kutojiunga au kubatilisha uanachama katika chama cha wafanyakazi na kukomesha kuhusika katika shughuli halali za chama cha wafanyakazi kama masharti ya ajira. Hivyo pia, mwajiri hawezi kumbagua mfanyakazi (kwa hatua ya kisheria au kufutwa kazi) kwa sababu ya unachama wa mfanyakazi katika chama cha wafanyakazi au kuhusika katika shughuli halali za chama cha wafanyakazi.

Mtu yeyote mwenye umri wa miaka kumi na saba na zaidi anaweza kuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi isipokuwa katiba ya chama hicho cha wafanyakazi iwe na toleo kinyume na hicho.

chanzo: §20 ya Katiba ya Zanzibari 1984; § 4-5 ya Sheria ya Mahusiano ya Kazi Nambari 1 kati ya 2005; §6-13 ya Sheria ya Vyama vya Wafanyakazi, 2001

Uhuru wa makubaliano ya hiyari

Haki ya maafikiano ya pamoja yamehakikishwa chini ya Sheria ya Mahusiano ya Kazi. Kila chama cha wafanyakazi ambacho kimeidhinishwa kuzungumza kwa niaba ya wanachama wake kwa lengo la maafikiano ya pamoja kina haki ya kuzungumza kwa pamoja  na mwajiri au shirika la wafanyakazi kuhusiana na mishahara, sheria na masharti ya ajira, mahusiano kati ya wahusika na masuala mengine ya pamoja. Maafikiano ya pamoja yanaweza kufanyika katika kiwango cha biashara, viwanda au kiwango cha sekta na kiwango cha kitaifa.

Makubaliano ya pamoja yaliyotiwa saini kati ya chama cha wafanyakazi na mwajiri mmoja yanamfunga mwajiri na wafanyakazi ambao ni wanachama wa chama hicho cha wafanyakazi katika kitengo cha mazungumzo. Wanachama wasio kwenye chama wanachukuliwa kuwa wamewakilishwa ambapo wengi wa wafanyakazi katika kitengo cha mazungumzo ni wanachama wa chama cha wafanyakazi katika makubaliano ya pamoja. Makubaliano ya pamoja lazima yasajiliwe. Huenda makubaliano ya pamoja yakahitimishwa na muda uliowekwa au muda usiojulikana. Makubaliano yote ya pamoja lazima yawasilishwe Mahakamani na nakala kwa Tume na mhusika yeyote ili kusajiliwa.

Haki ya makubaliano ya pamoja hutolewa kwa wafanyakazi wote isipokuwa maafisa wa umma wanaohusika katika kusimamia serikali, na wafanyakazi wakuu katika kusimamia masuala ya wafanyakazi.

chanzo: §54-61 ya Sheria ya Mahusiano ya Kazi Nambari 1 kati ya 2005; §52 ya Sheria ya Vyama vya Wafanyakazi, 2001

Haki ya Kugoma

Haki ya kugoma (na njia ya wafanyakazi kutofanya kazi) inatambuliwa nchini Zanzibari. Hata hivyo haki ya kugoma inaweza kutekeleza tu kwa mizozo ya matakwa na wala sio mizozo ya haki. Katika hali ya mgomo, notisi ya mapema iliyoandikwa ya saa 48 lazima iwasilishwe kwa mwajiri kabla ya kuanza mgomo (ilani ya mapema ya siku saba ikiwa serikali ndio mwajiri). Wafanyakazi katika vyeo vya usimamizi na hata pia wale wanaohusika katika huduma muhimu, kati ya kazi nyingine, hujumuisha maji na usafi, umeme, huduma za afya, wadhibiti wa trafiki ya ndege, huduma za moto, na huduma za uchukuzi. Mwajiri hawezi kuwabadilisha wafanyakazi kabisa wakiwa katika mgomo halali (au hata kuanzisha mashtaka ya nidhamu dhidi ya mfanyakazi anayehusika katika mgomo halali) hata hivyo anaweza kutafuta wafanyakazi wa muda wa kushikilia wafanyakazi wanaogoma ili watoe huduma za udumishaji na huduma nyingine muhimu (ikiwa sheria husika imetolewa na Waziri wa Kazi).

chanzo: 62-71 ya Sheria ya Mahusiano ya Kazi Nambari 1 ya 2005; §107 & 118 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005

loading...
Loading...