Ukaguzi wa mahali pa kazi

Yote kuhusu ukaguzi wa mahali pa kazi, ukaguzi wa mahali pa kazi na uhusiano wa mwajiri na mwajiriwa mahali pa kazi na sheria za kazi katika Mywage Tanzania

Ni nini ukaguzi chini ya Sheria ya Taasisi za Kazi ya mwaka 2004?
Ukaguzi unaweza kuelezewa kama kitendo cha kukagua eneo la kazi kinachofanywa na Afisa Kazi kuangalia kama sheria za kazi zinafuatwa na kuzingatiwa na mwajiri. Kuna sheria kadha zinazowawezesha maafisa kufanya ukaguzi mahali pa kazi. Makala hii itaangalia ukaguzi unaofanywa na na Maafisa Kazi wenye mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa sheria za kazi chini ya sheria ya Taasisi za Kazi Na. 6 ya mwaka 2004.

Je Afisa Kazi anaweza kutembelea eneo la kazi kwa ajili ya ukaguzi bila ya kutoa taarifa za awali?
Ndio. Afisa Kazi haitaji kutoa taarifa za awali kabla hajatembelea eneo la kazi kwa ukaguzi, kwa maana ili waweze kupata taarifa sahihi wanahitajika kutembelea bila kutoa taarifa ama kwa kushtukiza. Kama taarifa za awali zitatolewa kuna uwezekano mwajiri akajipanga kwa kuficha mambo kadha ambayo yanaenda kinyume cha sheria. Sheria inahitaji ukaguzi ufanyika katika muda unaofaa. Hata hivyo sheria inamuhitaji Afisa Kazi kua na cheti husika chenye kumhalalisha.


Je Afisa Kazi anaweza kuchukua vitabu, taarifa na vitu vingine wakati wa ukaguzi?
Afisa Kazi anaweza kufanya upekuzi na kutathmini taarifa yoyote, kitabu, nyaraka au kitu chochote halisia kama kinahusika/kupatikana, kuvizuia kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Wanaweza pia kuchukua sampuli ya kitu chochote kilichopatikana, kuchukua vipimo, masomo, rekodi au picha na kumhoji mtu yeyote aliye katika eneo hilo. Afisa Kazi atahitajika kutoa risiti kwa kitabu, nyaraka au kitu chochote halisia alichokichukua kuelezea vilivyochukuliwa.

Mwajiri wangu ameitwa na Afisa Kazi lakini amekataa kukutana nao. Je kuna adhabu yoyote?
Kifungu cha 45 (1) (b) kinampa Afisa Kazi mamlaka ya kutoa agizo kwa mtu yeyote kuja kwa tarehe elekezi ili kuweza kumhoji. Mtu huyu pia anaweza kuhitajika kutoa maelezo zaidi juu ya taarifa, kitabu, nyaraka au kitu chochote halisia na kuelezea yoyote yaliyomo katika hivyo. Pale itakapotokea mwajiri amekataa wito wa Afisa Kazi au kutoa taarifa au nyaraka Afisa Kazi anaweza kufungua mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi au Wilaya na kumshtaki kwa niaba ya Kamishna wa Kazi. Makosa kadhaa yanaweza kutendwa dhidi ya Afisa Kazi ikiwemo kukinza au kumzuia afisa kazi kutekeleza utendaji kazi au anapotumia mamlaka ya kiafisa, kukataa au kushindwa kujibu, bila ya sababu za msingi swali lolote alilohoji afisa wa kazi kwa mujibu wa kifungu cha 45(1)(a)(vi) au (1)(c) na mengine yameorodheshwa katika kifungu cha 49 cha sheria ya Taasisi za Kazi ya mwaka 2004.

Je afisa kazi anahitajika kufanya nini kama atagundua hakuna utekelezaji na uzingatiaji wa sheria mahali pa kazi?
Afisa wa kazi akiamini kuwa na sababu za msingi kwamba mwajiri hakutekeleza matakwa ya vifungu vya sheria ya kazi anaweza kutoa amri tekelezi kwenye fomu ya agizo. Amri tekelezi hii pia inaweza kutolewa wajumbe wa chama chochote cha wafanyakazi kilichosajiliwa ambao wajumbe wake ni kati ya wafanyakazi wataaoathiriwa na amri hii. Mwajiri anaweza akapinga kwa maandishi amri tekelezi iliyotolewa kwa mujibu wa kifungu cha 46 ndani ya siku 30 tangu kupokelewa kwa amri hiyo kwa kuwasilisha pingamizi kwa Kamishna wa kazi. Kamishna wa kazi atapeleka maombi kwenye Mahakama ya Kazi ili kutekeleza amri tekelezi ikiwa kama mwajiri hajaitekeleza na hajatoa pingamizi lolote dhidi ya amri hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 47(1) cha sheria ya Tasisi za Kazi ya mwaka 2004.

Itakuaje kama Kamishna atapuuzia pingamizi la mwajiri?
Kama pingamizi litapuuziwa na Kamishna wa Kazi, mwajiri anaweza kukata rufaa Mahakama ya Kazi. Kwa maombi ya mwajiri Mahakama ya Kazi kulingana na makubaliano na masharti inaweza ikasimamsisha amri ya Kamishna wa Kazi mpaka pale amri ya mwisho ya Mahakama ya Kazi au rufaa yoyote dhidi ya maamuzi ya Mahakama ya Kazi. Mahakama ya Kazi inaweza ikathibitisha, ikabadilisha au ikafuta amri, na amri liliyothibitishwa, iliyobadilishwa au kufutwa italazimu kuainisha kipindi ambacho mwajiri anapaswa kufuata amri iliyothibitishwa au iliyobadilishwa.

Soma zaidi

Fahamu zaidi kuhusu sheria za kazi za Tanzania. Jaza tafiti yetu ya Mishahara

loading...
Loading...