Haki ya Chama

fahamu yote juu ya haki ya chama cha wafanyakazi na sheria isemavyo, pata yote na zaidi katika mywage.org/tanzania

Ni zipi haki za kichama?

Haki za kichama ni haki za chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa kufanya yafuatayo:
•    Kutafuta wanachama
•    Kuwasiliana na wanachama
•    Kukutana na wanachama katika kumshughulikia mwajiri.
•    Kuendesha mikutano na wafanyakazi katika majengo ya mwajiri.
•    Kupiga kura chini ya katiba ya chama.
Haki hizi zinaelezewa katika kifungu cha 60 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004. Chama kilichosajiliwa kinaweza kuanzisha tawi la nje ya sehemu ya kazi ambayo watu kumi au zaidi wameajiriwa na watakua na haki ya kupata likizo kwa ajili ya shughuli za chama. 

Je haki za kichama ni haki za lazima kwa wajumbe wa chama cha wafanyakazi?

Haki za kichama ni haki zako lakini ni lazima zitekelezwe kwa maadili ili kuhakikisha kwamba zinafuata utaratibu na haziingilii utendaji wako wa kazi. Kifungu cha 64 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 inakitaka chama cha wafanyakazi kinachokusudia kutumia haki zake kumtaarifu mwajiri kwa kupitia fomu maalumu juu ya makusudio ya kutumia haki zake. Kushindwa kufanya hivyo kunaweza kupelekea mwajiri kukataa maombi hayo. 

Nini kitatokea kama chama cha wafanyakazi kitavunja kwa kiasi kikubwa masharti ya utekelezaji wa haki za chama?

Inapotokea uvunjifu wa kiasi kikubwa cha masharti ya utekelezaji wa haki za chama, mwajiri anaweza kupeleka suala hilo kwenye Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA). Kama Tume itashindwa kutatua mgogoro mwajiri anaweza kuiomba Mahakama ya Kazi ambayo inaweza kubatilisha haki yoyote ya chama iliyopewa chama cha wafanyakazi. 

Nini kitatokea kama mwajiri atakataa kukutana na chama cha wafanyakazi kwa ajili ya kujadili haki za chama?

Kama chama cha wafanyakazi kitatimiza mahitaji yote ya muhimu kiasi cha kustahili haki za chama, mwajiri hatokua na haki za kukataa kutoa haki hizo; japo zinaweza kutolewa kwa masharti. Kama mwajiri atakataa kukutana na chama cha wafanyakazi ndani ya siku 30 toka siku alipopokea taarifa au kukataa kutoa haki za chama bila sababu za msingi chama cha wafanyakazi kinaweza kupeleka mgogoro kwenye Tume ya Usuluhishi na  Upatanishi. 

Mimi ni mwakilishi wa chama cha wafanyakazi katika mahali pangu pa kazi, Je ni sawa kwa mwajiri kuninyima muda wa malipo wa ziada wa kusafiri kwa ajili ya kufanya shughuli za chama?

Sheria inakuruhusu kupewa muda wa malipo wa ziada ili kufanya mambo ya msingi yafuatayo:
•    Kuwakilisha wanachama katika malalamiko na mashauri yahusuyo nidhamu;.
•    Kutoa uwakilishi kwa niaba ya wajumbe kuhusiana na kanuni; afya na usalama na hali nzuri;.
•    Kushauri juu ya uzalishaji katika sehemu ya kazi;.
•    Kukiwakilisha chama cha wafanyakazi katika uchunguzi na upelelezi unaofanywa na wapelelezi kwa mujibu wa sheria zozote za kazi;
•    Kumwangalia mwajiri kama anafuata sheria za kazi;
•    Kufanya kazi za chama cha wafanyakazi chini ya katiba ya chama;
•    Kuendeleza uhusiano mzuri;
•    Kufanya kazi nyingine au wajibu uliokubaliwa na mwajiri.
Itakapotokea kwamba moja kati ya haki zilizotajwa hapo juu zimekataliwa na mwajiri bila sababu za msingi basi mwakilishi wa chama cha wafanyakazi anaweza kupeleka suala hilo Tume ya Usuluhishi na Upatanishi. 

Je chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa kinahitajika kua na wawakilishi wangapi katika mahali pa kazi?

Chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa kitakua na haki za:
•    Mwakilishi mmoja kuanzia mjumbe mmoja kwa wajumbe tisa;.
•    Wawakilishi watatu kwa wajumbe kumi hadi ishirini;.
•    Wawakilishi kumi kwa wajumbe ishirini na moja hadi mia moja;.
•    Wawakilishi kumi na tano katika sehemu za kazi ambazo zina zaidi ya wajumbe mia moja.

loading...
Loading...