Kuitisha Migomo

Fahamu zaidi kuhusu taratibu za kuitisha migoma sehemu za kazi na nini sheria inasema kuhusu migomo. Je mwajiri ana haki ya kukataza migomo au kufukaza wafanyakazi waliogoma? Fahamu yote haya kupitia www.mywage.org

Migomo na taratibu za kuiitisha
Kuitisha mgomo ni haki ya kila mtumishi, lakini wakati Fulani mahakama hutangaza kuwa baadhi yamaandano siyo halali kwa kuwa hayafuati sheria,licha ya kuwa maandano hayo yameruhusiwa kwenye sheria ya kazi. Hii ni kwasababu ya ukweli kwamba chama husika cha wafanyakazi kimeshindwa kuzingatia taratibu zilizowekwa kisheria. Hii ni kwasababu ya kutojua sheria au kukosa subira. Hii ndio sababu ni muda mwafaka kujadili suala hili na taratibu zinazotakiwa kufuatwa, ili kuepuka ukiukwaji wa sheria usio na msingi, kutozwa faini, na watumishi kushindwa kudai haki zao.


Je,mgomo ni nini?
Sheria inaeleza kuwa mgomo ni kususia au kutega kufanya kazi kunakofanya na watumishi, iwapo kususia huko ni kutaka kushinikiza mwajiri, au hata Waajiri wengine au chama anachoshiriki mwajiri ilikuridhia, kurekebisha, au kutengua madai yoyote yanayochochea watu kuingia kwenye mgomo.
Watumishi wanaweza kugoma endapo wanamgogoro wa kimasilahi. Mgogoro wa kimasilahi ni mgogoro unaohusu haki ya siku za usoni au maombi yahusuyo taratibu za ajira tofauti na zile zinazotolewa katika mkataba wa kazi kisheria, kwa mfano, kuongeza mshahara.


Je, ni kweli kwamba naruhusiwa kugoma kisheria?
Ndio, Sheria inaweka wazi kuwa kila mtumishi ana haki ya kugoma kama kuna mgongano wa kimasilahi; lakini mgomo huo sharti uitishwe na chama kinacho wakilisha umoja wa wafanyakazi.

Hata hivyo kuna mazingira fulani ambapo mgomo hauruhusiwi:
•    Iwapo mtumishi ameajiriwa kwenye kutoa huduma nyeti na hakuna sheria au makubaliano yaliyofikiwa ili kupunguza huduma kipindi cha mgomo. Huduma nyeti zimeorodheshwa kisheria kama vile maji na usafi, umeme, huduma ya afya, maabara, zima moto, huduma ya anga, mawasiliano, na aina yoyote ya usafiri iliyoko chini ya kundi la huduma muhimu.
•    Iwapo mtumishi ameajiriwa kwenye huduma ya kiwango cha chini.
•    Iwapo mtumishi anabanwa na makubaliano yanayomtaka aende kwenye usuluhishi.
•    Iwapo mtumishi anabanwa na makubaliano ya pamoja au usuluhishi uliofikiwa   unaolenga kumaliza mgogoro.
•    Iwapo mtu huyo ni hakimu, mwanasheria, au afisa yeyote wa mahakama.
•    Iwapo suala husika si mgogoro badala yake ni malalamiko.


Ni taratibu zipi za kufuata kabla ya kuitisha mgomo?
Awali ya yote mgogoro sharti uwe wa kimasilahi na uwe umepelekwa kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi. Kama chombo hicho kitashindwa kutatua mgogoro huo basi italazimu kuitisha mgomo.
Mgomo unatakiwa uitishwe baada umoja wa watumishi baada ya kura kupigwa na kuonekana kuwa wengi wanakubaliana na kuingia kwenye mgomo.
Umoja huo unatakiwa kumtumia notisi mwajiri ndani ya saa 48 ukimfahamisha kuhusu kusudi la kuitishamgomo.Notisi hiyo itolewa baadaya Maridhiano naUsuluhishi kushindwa.
Iwapo notisi ya saa 48 imeshatolewa na kupita muda wake basi umoja unaweza kuitisha mgomo.


Je,kuna madhara yoyote endapo taratibu zilitajwa hazitafuatwa?
Iwapo mgomo haujafuata taratibu zilizotajwa kisheria Mahakama ya Kazi ina mamlaka ya kutangaza kuwa mgomo huo ni batili kwa kutoa amri inayokataza mtumishi yeyote kushiriki katika mgomo batili. Mahakama pia inaweza kuamuru kutoa fidia kwa hasara itakayotokana na mgomo. Sheria pia inaamuru kusitishwa kwa ajira ya watumishi watakaoshiriki katika mgomo batili.


Je, sheria inaruhusu mwajiri kusitisha mshara wangu wakati wa mgomo?
Mwajiri habanwi kisheria kuendelea kulipa mshahara kwa mtumishi anayeshiriki katika mgomo. Kama mwajiri unatakiwa uendelee kuchangia kwenye mfuko wa jamii na mchango utakatwa kwenye mshahara wa mtumishi baada ya mgomo.

 
Ni vitendo gani vingine vinakatazwa wakati wa mgomo?
Vitendo vifuatavyo vinavyohusishwa na mgomo vimekatazwa kisheria:
•    Kuzingira mahali pa kazi.
•    Kufanya kazi muda wa ziada dhidi ya mwajiri.
•    Kumfungia mwajiri kwenye mazingira ya kazi.
•    Kumzuia mwajiri asiingie mahali pa kazi.

Soma Zaidi
loading...
Loading...