Kazi na Ujira

This page was last updated on: 2021-01-20

Kima cha Chini cha Mshahara

Kulingana na katiba ya Tanzania, kila mtu, bila ubaguzi wa aina yeyote, ana haki ya kupata ujira kutokana na kazi na wote wanaofanya kazi, wanapaswa kupata stahiki zao za malipo kwa kadiri ya utendaji na sifa za kufanya kazi husika. Kila mtu ana haki ya kupata malipo stahiki.

Viwango hivi huwekwa na Bodi za mishahara za kisekta ambazo zipo kwa mujibu wa Sheria ya kazi ya mwaka 2007. Ili kufikia viwango vya chini vya mshahara, bodi za mishahara za kisekta huzingatia vigezo muhimu kama vile gharama za maisha; hali ya mishahara nchini; uzalishaji; uwezo wa waajiri kuendesha biashara zao vizuri utekelezaji kazi wa shughuli za kibiashara za kati; ndogo na ndogo sana; biashara mpya; gharama za kuishi; kupunguza umaskini; kiwango cha chini cha kujikimu; malipo na makubaliano na masharti ya ajira kwa waajiriwa wa sekta ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Makubaliano yoyote ya pamoja ya malipo na mapatano na masharti ya ajira kwenye sekta. Tukio la sharti lolote la ajira lililopendekezwa kwa ajira ya wakati huo au uuandaaji wa ajira.

Kwa sasa kuna viwango vya chini vya mshahara kwa sekta zifuatazo: Ujenzi, shule binafsi, nishati, viwanda na biashara, hoteli na huduma za majumbani, Nyingine ni ulinzi binafsi, madini, afya, uvuvi, usafirishaji, mawasiliano na kilimo na nyingine zisizo tajwa hapa.

Idara ya Usimamizi na ukaguzi wa kazi, iyopo ofisi ya Waziri Mkuu husika na, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi ,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu ndiyo yenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa kima cha chini cha msharaha kwa wafanyakazi, hususani, wa Sekta Binafsi. Maasifa wa Kazi wa idara hii, wanapewa mammlaka na Sheria ya Taasisi ya Kazi, yam waka 2004, kusimamia utekelezaji wa viwango vya kazi, ikiwa ni pamoja na kima cha chini cha mshahara, kama kilivyo kubaliwa kwa mujibu sheria.

Inapotambulika, mwajiri hatekelezi matakwa ya kisheria, Afisa wa kazi atatoa sharti la kumtaka mwajiri husika kutekeleza matakwa ya kisheria ndani ya kipindi maalumu. Endapo atakaidi, atafunguliwa mashtaka na endapo atakutwa na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi za kitanzania milioni tano au kufungwa jela kwa kipindi cha miezi mitatu, au vyote kwa pamoja.

Vyanzo: § Sehemu ya 23 ya Katiba ya Tanzania; § Sehemu ya 37 na 64 (2) ya Sheria za Taasisi za Wafanyakazi ya 2004 ; §14-18 ya Sheria za Ajira na Kazi (Marekebisho ya Ziada), 2015

Kwa kima cha chini kilichosasishwa cha mshahara, rejelea sehemu ya Kima cha Chini cha Mshahara.

Malipo ya kawaida

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 hutofautisha kati ya "ujira" na "mshahara wa kawada". Ujira ni thamani kamili ya malipo yote, kipesa au kwa njia yoyote, inayolipwa mfanyakazi kutokana na ajira ya mfanyakazi huyo. Mshahara wa kawaida humaanisha sehemu ya ujira wa mfanyakazi huo unaolipwa kuhusiana na kazi iliyofanywa wakati wa saa za kawaida za kufanya kazi lakini haijumuishi marupurupu (iwe inategemea mshahara wa kawaida wa mfanyakazi au la) na malipo ya kazi ya ziada.

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini husimamia malipo ya mishahara kwa wafanyakazi wa aina yoyote. Kulingana na Sheria hii, mishahara inaweza kuhesabiwa kwa saa, kila siku, kila wiki, au kila ,wezi. Wafanyakazi walioajiriwa mara kwamara badala ya muda wa kufanya kazi hulipwa kila wiki na mishahara yao uhesabiwa kwa msingi wa kiwango wastani ulichokipata kwa kipindi cha wiki 13 au kulingana na muda wao wa ajira (ikiwa ni chini ya wiki 13).

Waajiri wanawajibika kumlipa mfanyakazi mshahara wake wa saa alizofanya kazi katika eneo la kazi kulingana na siku ya malipo katika bahasha iliyofunika, ikiwa malipo yatakuwa kwa pesa taslimu au kupitia cheki.  Mshahara unaweza kuweka moja kwa moja kwenye akaunti iliyoteuliwa na mfanyakazi kwa kuandikwa. Waziri anayewajibika kwa masuala ya kazi anaweza kuruhusu malipo nusu ya mshahara kwa matumizi ya kibinafsi kwa mfanyakazi na familia yake.

Kwa ujumla, mwajiri haruhusiwi kupunguza mishahara isipokuwa iki inahitajika au imeruhusiwa chini ya sheria iliyoandikwa, makubaliano ya pamoja, uamuzi wa mshahara, agizo la mahakama au tuzo la maombi ya rufaa. Kipunguzo kinaweza pia kufanywa ikiwa mfanyakazi atakubali kipunguzo hicho kwa kuandika kuhusiana na deni au kumfidia mwajiri kwa hasara au uharibifu uliosababishwa na mfanyakazi. Kiwango cha jumla cha kipunguzo lazima kisiwe zaidi ya robo nusu ya ujira wa mfanyakazi.

Mwajiri anastahili kutoa risiti za malipo kwa wafanyakazi wote pamoja na malipo ya pesa taslimu au cheki; au kumpa mfanyakazi katika bahasha iliyofungwa iwapo ni pesa taslimu. Sehemu ya 12 ya Kanuni kuu za Sheria ya Ajira na mahusioano kazini, kama zilivyo rekebishwa mwaka 2017, inatoa maelezo toshelezi ya taarifa za kuwepo kwenye hati ya mshahara.

Vyanzo: Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Taratibu juu ya Kazi na Ujira

  • Sehemu ya tano ya Sheria ya Kanuni za Ajira na Mahusiano kazini namba 7 ya 2004 (kupitia Taratibu zamishahara na kanuni za Ajira (The Wage Order)) / Part V of Labour Institutions Act, No.7 of 2004 (through Regulation of Wages and terms of Employment Order, 2013 aka The Wage Order)
  • Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004 / Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004
  • Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (imefanyiwa marekebisho mwaka 1995) / The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 (amended in 2005)
loading...
Loading...