Udhalilishaji kijinsia Mahali pa Kazi

This page was last updated on: 2021-01-20

Udhalilishaji kijinsia Mahali pa Kazi

Unyanyasaji kijinsia mahali pa kazi ni ubaguzi na umekatazwa kisheria na ni sehemu ya Kanuni za adhabu.

 Anayekutwa na hatia ya kufanya hivyo, ataweza kupata kifungo cha hadi miaka mitano, au faini isiyozidi shilingi laki mbili au vyote kwa pamoja, na pia anaweza kupewa amrisho la kulipa fidia kwa aliyeathirika kama itakavyo amriwa na mahakama

Matendo ya ngono yatakayo sababishwa kwa maneno au matendo na mtu aliye na madaraka katika sehemu ya kazi au sehemu nyingine yoyote, atakuwa ametenda kosa la udhalilishaji wa kijinsia. Hakuna shtaka kwa kosa chini ya kifungu hiki litaanzishwa au kuendelea ikiwa lalamiko hilo litafanywa na mlalamikaji wakati wowote baada ya siku sitini tangu kutokea tukio lililosababisha kosa.

Chanzo: §7 Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini 2004; § ya 138 (D) ya kanuni za adhabu, 1945

loading...
Loading...