Utumikishaji wa Watoto

This page was last updated on: 2021-01-20

Watoto chini ya miaka 15

Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Kazi, 2004, mtoto chini ya miaka 14 hapaswi kuajiriwa. Mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi tu, ambazo haziwezi kuwa na madhara kwa afya ya mtoto na maendelo yake. Uajiri wa mtoto kamwe usimzuie mtoto kuhudhuria masomo shuleni, kushiriki kwenye ufundi stadi au miradi ya mafunzo yaliodhibitishwa na mamlaka yenye madaraka au uwezo wa mtoto kufaidi maelekezo anayoyapata.

Katiba ya Tanzania inatoa ufikiaji sahihi ili kufikia elimu na kila mwanainchi ako huru kutafuta masomo na uwezo wake na kulingana na uwezo wao.

Mtoto haruhusiwi kufanya kazi wakati was aa za shule. Na mtoto anaye endelea na masomo, haruhusiwi na hapaswi kufanya kazi kwa Zaidi ya masaa matatu kwa siku. Mtoto wa umri wa miaka 14 na Zaidi na anapokuwa likizo au amekwisha hitimu elimu ya msingi, au hasomi kwa sababu mbali mbali za msingi, anaweza kuajiriwa kufanya kazi kwa kipindi kisicho zidi masaa 6 kwa siku. Mtoto asiruhusuiwe kufanya kazi kwa masaa matatu mfululizo bila ya walau saa moja ya mapumziko.

Chanzo: §5 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Kazi, 2004; §11 ya katiba ya Tanzania; §3-10 ya Kanuni kuu za sheria ya Ajira na mahusionao, 2017

Umri wa chini kwa kazi hatarishi

Umri wa chini kwa kazi hatarishi ni miaka 18. Mtu yeyote haruhusiwi kumwajiri mtoto kwenye ajira- (a) ambayo haifai kwa mtu mwenye umri huo; (b) sehemu ambayo inayohatarisha hali nzuri ya mtoto, elimu, afya ya mwili na akili, au roho, maadili au maendeleo ya kijamii. Mtu anaye ajiri mtoto kwenye kazi yeyote inayo ashiria utumikishwaji wa watoto anafanya kosa na atakapo kutwa na hatia, anaweza kupata adhabu isiyo pungua faini ya shilingi laki moja au kifungo cha miezi mitatu au vyote.

Ni kinyume na sheria kwa mtu yeyote kuajiri mtoto katika aina ya kazi hatarishi. Kazi yeyote ambayo inaweza kupelekea adhari za kiafya, usalama au maadili ya mtoto ni hatarishi. 

Kazi hatarishi ni pamoja na Kazi za kwenye vyombo vya majini kama vile meli, migodini, kubeba mizigo (kuli), kazi za viwadani ambako kemikai zina zalishwa au kutumika, kazi zinazotumia mashine, kazi kama vile za vilabu vya pombe (bar), nyumba za wageni (hotels), na sehemu za starehe. Kazi za usiku (kati ya 2 na 12 usiku) na saa za ziada za kazi haziruhusiwi kwa watoto. Kanuni za Ajira na mahusiano, 2017 zime orodhesha kazi hatarishi zilizo marufuku kwa watoto wa chini ya miaka 18.

Chanzo: § 5(3) ya Sheria za Kazi na Ajira, 2004; § 77-86 ya Sheria ya Ajira ya Mtoto ya 2009; §3(2) na jedwali la kwanza la Kanuni za Ajira na mahusiano, 2017

Taratibu dhidi ya Utumikishaji wa Watoto

  • Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004 / Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004
  • Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (imefanyiwa marekebisho mwaka 1995) / The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 (amended in 2005)
  • Sheria ya Haki za Mtoto, 2009 / Law of the Child Employment Act, 2009
loading...
Loading...