Uzazi na Kazi

This page was last updated on: 2021-01-20

Likizo ya Uzazi

Likizo ya uzazi inatolewa na kudhibitiwa chini ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini 2004.

Wafanyakazi wanawake wana haki ya angalau wiki kumi na mbili (siku 84) ya likizo ya uzazi au siku 100 mfululizo (katika hali ya mapacha) na kuendelea kupata mshahara katika kipindi cha likizo cha miezi 36. Mfanyakazi anahaki ya siku 84 za likizo ya uzazi katika kipindi cha likizo ikiwa aliyezaliwa karibuni atafariki ndani ya mwaka wa kuzaliwa.

Mfanyakazi mja mzito lazima ajulishe mwaji na atoe cheti cha matibabu miezi 3 kabla ya kuendelea na likizo ya Uzazi. Anaweza kuanza likizo ya uzazi wiki nne kabla ya tarehe ya uangalizi au mapema ikiwa daktari atadhibitisha ya kwamba ni muhimu kwa mfanyakazi au mtoto wake. Pia, mfanyakazi haruhusiwa kufanya kazi ndani ya wiki 6 ya kuzaliwa kwa mtoto ila tu daktari amruhusu.

Mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi likizo ya uzazi na kumlipa mara nne wakati wa huduma yake.

Chanzo: § 33 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Mshahara

Mfanyakazi atapata mshahara wake kamilifu kipindi awapo katika likizo ya uzazi. Malipo haya hulipwa na mwajiri .

Sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii, inaruhusu mfanyakazi kulipwa takribani mshahara wa majuma 12 kabla ya juma la 20 la ujauzito. Pesa hizo zinawezwa kukipwa kwa awamu mbili: wiki nne kabla ya kujifungua na wiki nane baada ya kujifungua (wiki nne baada ya kujifungua, endapo mtoto amefariki).

Chanzo: §33 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004, § ya 45(b) ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 1997; ISSA Nchi ya Tanzania, 2017

Huduma ya bure ya matibabu

Kwa mujibu wa sheria, mwanamke ana haki ya uangalizi kiafya kabla na baada ya kujifungua, ikiwa ametoa angalau michango thelathini na sita ya kila mwezi ambapo michango kumi na miwili imefanywa miezi thelathini na sita kabla ya tarehe ya uangalizi. Ruzuku ya uzazi inatolewa baada ya upokezi wa cheti cha tiba na Mkurugenzi Mkuu kutoka kwa daktari, ikiidhinisha ya kwamba mwanamke anatarajia kujifungua mtoto

Chanzo: §44-45 ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 1997 

Taratibu juu ya Uzazi na Kazi/Regulations on maternity and work

  • Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004 / Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004
  • Sheria ya Mfuko wa Hifandhi ya Taifa ya Jamii (NSSF) Mwaka, 1997 / National Social Security Fund Act, 1997
loading...
Loading...