Kazi za kufanyia nyumbani

fahamu kuhusu kazi za kufanyia nyumbani na sheria za kazi tanzania kupitia mywage Tanzania

Kazi za nyumbani ni nini?

Kazi za nyumbani hujumuisha kundi la kazi rasmi na zile zisizo rasmi ambapo mtu hufanya kazi akiwa nyumbani au karibu na nyumbani bila kwenda kwa mwajiri.
Kazi za nyumbani ni moja ya mfumo wa zamani ambao historia yake imeanzia Kusini mwa Bara la Asia. Katika dunia ya utandawazi, kazi za nyumbani zimeimarika na kutoa faida kubwa kwa makampuni. Kazi hizo zina faida hususan kwa kina mama ambao hawahitaji kwenda nje na hivyo kuunganisha kazi hizo na zile za kawaida zisizo na malipo wakati huo huo wakibakia nyumbani.

Kazi zipi si za nyumbani?

Kazi za nyumbani hazihusishi shughuli za nyumbani zinazofanywa bila malipo kama sehemu ya wajibu katika familia au zile zinazofanywa kwa  malipo kama vile kufua, kufanya usafi, kulea mtoto, safisha, na kadhalika. Kazi za nyumbani sharti zimwezesha mtu kujipatia kipato na lazima zisiwe zimefanyika katika mazingira ya mwajiri, badala yake zinatakiwa zifanyike nyumbani au karibu na mazingira ya maskani.

Je, kuna kadirio lolote la jumla ya kazi za nyumbani ulimwenguni?

Watumishi wa nyumbani huunda sehemu kubwa ya wafanyakazi dunia katika viwanda nyeti kama vile vya nguo, ngozi, na  mazulia na vile vile katika taasisi za kiasasa madhalani masuala ya umeme. Kazi hizo hupatikana katika mataifa yaliyoendelea nay ale yanayoendelea kama vile Pakistan, Bangladesh, India na kadhalika.
Kutokana na kukua kwa teknolojia, kazi za nyumbani zimekuwa kwa kiasi kikubwa si tu katika uzlishaji bali pia katika utoaji huduma ambapo madhalani mwanasheria huweza kutoa msaada akiwa nyumbani, mganga huweza kutibu akiwa nyumbani kwa baadhi ya mataifa, mwandishi wa habari huweza kufanya kazi zake nyumbani na kadhalika. Inakadiriwa kuwa kuna takriban wafanyakazi wa nyumbani  milioni 100, zaidi ya nusu yao wako Barani Asia Kusini wakati karibu asilimia 80 ya wafanya kazi hawa milioni 50 ni wanawake.

Kutokana na makadirio ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), zaidi ya asilimia 10 mpaka 25 ya shughuli za kilimo katika mataifa yanayoendelea ni miongoni mwa kazi za nyumbani  wakati idadi hiyo ni karibu  asilimia 4 mpaka 11 katika mataifa yenye uchumi uliostawi.

Nini kimesababisha kuongezeka kwa kazi za nyumbani?

Kuna sababu kuu tatu za kuongezeka kwa kazi za nyumbani. Kwanza, utandawazi umeongeza msukumo kwa makampuni kupunguza gharama kupitia uzalishaji kwa njia ya mkataba na kuhamasisha mikataba inayoweza kufanyiwa mabadiliko.
Pili, teknolojia ya habari imewarahisishia wafanyakazi hasa wale wenye utaalamu na wale wenye ujuzi mkubwa  kufanyia kazi nyumbani. Tatu,  ukosefu wa fursa za kazi rasmi kutokana na kudorora kwa uchumi hususani katika sekta ya fedha kumesababisha watu kuamua kujiajiri nyumbani. Sababu hizi zote zimechangia kuongeza kwa watumishi wa nyumbani.

Je, ni aina ngapi tofauti za wafanyakazi wa nyumbani?

Kuna aina mbili za watumishi wa nyumbani. Watumishi wa mikataba mifupi hawa humfanya kazi na mwajiri na mtu wa katikati  wakati Wanaojitegemea kifedha ni wale wanaofanya kazi kwa kujitegemea na kwa kujitafutia masoko wenyewe.

Watumishi wa mikataba mifupi

Watumishi wa aina hii hufanyakazi kwa mikataba mifupi na kulipwa kulingana na kile wanachozalisha. Watu hawa hawana uhusiano wa moja kwa moja na mauzo ya kile wanachokizalisha. Wanatakiwa pia kutafuta mali ghafi na zana nyingine muhimu zinazotakiwa katika uzalishaji. Watumishi hawa huajiriwa na makampuni ya kienyeji kama yale yanayazalisha na kuuza nguo, yale ya kimataifa mathalani ya mpira wa miguu.

Wanaojitegemea kifedha

Watumishi hawa hushughulikia moja kwa moja suala la masoko na kununua mali ghafi zao binafsi. Hawa hukabiliana na ushindani kutoka kwa makampuni makubwa na hawana njia rahsi ya kupata pesa. Kipato cha watu hawa ni kidogo na gharama ya uzalishaji kwao ni kubwa mno.

Je, kuna tofauti gani kati ya wale wanaofanyia kazi nyumbani na wafanyakazi wa nyumbani?

Watumishi wanaofanyiakazi nyumbani ina maana pana ambapo huhusisha wale wote wanaofanyia kazi nyumbani au karibu na nyumbani ikiwa ni wale wa mikataba mifupi, wale Wanaojitegemea Kifedha au wale waliojiajiri.
Kwa upande mwingine, watumishi wa nyumbani ni sehemu ndogo ya watu waliojiajiri majumbani na hawa kwa kawaida ni wale wanaofanya kazi za mikataba, na hufahamika pia kama watu watumishi wa nje ya mazingira ya kazi.


Je, shirika la kazi duniani linasema nini juu ya watumishi wanaofanyia kazi nyumbani?

Baada ya juhudi za muda mrefu za Chama cha Wanawake Waliojiajiri (SEWA) na Umoja wa Wafanyakazi wa nyumbani wa Kimataifa (HomeNet), mwaka 1996 Shirika la Kazi Duniani (ILO) lilianzisha kanuni yakusimamia kazi za nyumbani. Kanuni hiyo (C177)hueleza kuwa kazi za nyumbani ni “ Kazi zinazofanywa nyumani ambapo mtu anayefanya kazi hizo huitwa mfanyakazi wa nyumbabani”

1.    Katika mazingira yake ya nyumbani au katika mazingira yoyote mengine kulingana na chaguo lake kuliko kwenda kwa mwajiri;
2.    Kwa ajili ya ujira;
3.    Kinachopelekea kupata zao au huduma kulingana na mahitaji ya mwajiri, bila kujali anayetoa vifaa uzalishaji, zana muhimu na vitu vingine vilivyotumika”
Kanuni ya ILO hutofautisha kati ya kazi za kutegemea mkataba mfupi (mtumishi wa nyumbani) na mfanyakazi wa kujitegemea. Wafanyakazi hawa hutofautishwa kupitia kiwango cha kujitemea kikazi au kiuchumi.

Je, kanuni ya ILO kuhusu kazi za nyumbani inaweza kutumika kwa wafanyakazi wanaojitegemea kifedha?

Hapana, kanuni hiyo inawahusu wafanyakazi wa nyumbani/wale wanaofanyakazi kwa mikataba mifupi na halijihusishi wazi wazi na watu waliojiajiri majumbani.

Ni haki zipi zinaainishwa kupitia Kongamano la ILO?
Kanuni hii inamtaka kila mshiriki kuandaa na kutekeleza sera ya taifa kuhusu wafanyakazi wa nyumbani, ambapo sera hiyo itasimamia usawa  kati ya watumishi wa nyumbani na wale walioajiriwa kwa malipo katika maeneo yafuatayo: bargain
1.    Uhuru wa kujiunga na ushirika na makubaliano ya pamoja;
2.    Ulinzi dhidi ya ubaguzi  katika soko la ajira na kazini;
3.    Usawa katika malipo kwa kazi zenye thamani sawa;
4.    Kulindwa kisheria katika jamii;
5.    Kuwa salama kikazi na kiafya;
6.    Kupata mafunzo;
7.    Umri mdogo kabisa na ulinzi wa mama na mtoto.

Kanuni pia inaagiza kuwaweka watumishi wa nyumbani kwenye takwimu ya wafanyakazi kitaifa ili wawe sehemu ya nguvu kazi ya taifa. Zaidi ya hayo, kanuni hii inayataka mataifa yatakayoridhia utaratibu huu kuanzisha mfumo wa kukagua watu wanaofanyia kazi nyumbani.

Kwa nini watu wanaofanyia kazi nyumbani hawatambuliki?

Watumishi wanaofanyia kazi nyumbani kwa kawaida hawapo kwenye takwimu ya wafanyakazi. Zaidi ya hayo, kazi hizi huchukuliwa kuwa ni za kina mama na hivyo kuwa kufanywa na wanawake wengi. Akina mama wanaofanya kazi za nyumbani hujiita “Wanawake wa nyumbani” au “Wasioajiriwa” (hususani wanapoulizwa kuhusu shughuli za kiuchumi wakati wa sensa) hata wanapokuwa wanafanya kazi kwa muda mrefu.

Kazi hii haitambuliki kwa sababu hupatikana kati ya kazi za sekta rasmi na zile zisizo rasmi. Sheria za kazi kwa kawaida hutambua makundi mawili ya watumishi:

1.    Waajiriwa(watumishi wanaosimamiwa) na
2.    Waliojiajiri (watumishi wasiosimamiwa)

Wafanyakazi wa nyumbani kwa maana wale wanaofanya kazi kutegemea mikataba mifupi hukosoa mfumo huu wa sheria za kazi kwa kuwa hujipatia kipato kwa kufanya kazi za mkataba mfupi bila kusimamiwa mpaka kuunda asasi rasmi.Kwa sababu ya utata huu wafanya kazi hawa hubaki bila kutambulika wala kuhesabiwa kwa takwimu.  

Ipi miundo tofauti ya kazi zinazofanyika nyumbani?

Kazi za kufanyia nyumbani zimegawanyika katika makundi makuu mawili kwa maana zile za Kimila na za Kisasa. Kazi za nyumbani za mfumo wa kimila ni za kutumia nguvu nyingi wakati zile zile nyingine zinazofuata mfumo wa kisasa hutegemea taarifa, uweledi wa hali ya juu na shughuli za kitaalamu. Kazi kimila huhitaji kiwango cha chini cha ujuzi ikiwemo malipo kidogo na huhitaji uwepo wa mhusika wakati kazi za kisasa si tu kwamba ni ngumu bali pia huhitaji ujuzi wa hali ya juu na zina malipo ya kuridhisha.
Kazi mbalimabi za kufanyia nyumbani ni hizi:

Kazi za nguvu:
•    Kushona
•    Kufungasha
•    Ukusanyaji
•    Kusuka mikeka
•    Kutengeneza mpira
•    Kutengeneza viatu
•    Kutengeneza sabuni
•    Kusuka vikapu
•    Kutengeneza mifuko
•    Kufua
•    Kusuka nywele
•    Kushona viatu

Kazi za kisasa

•    Kuhifadhi takwimu
•    Kuhesabu
•    Kutafuta masoko
•    Kutoa ushauri wa kitabibu
•    Kujenga
•    Kushauri juu ya ushuru
•    Kutoa ushauri wa kisheria
•    Kuandika kwenye tovuti
•    Kutumia komputa

Jinsi gani tunatofautisha kati ya watumishi wa kazi za mkataba mfupi/watumishi wa nyumbani,watumishi wa kujitegemea kifedha/Waliojiajiri na waajiriwa?

Jedwali lifuatalo kutoka ILO linatofautisha kati ya aina hizi za wafanyakazi.

Muundo wa kazi      Waliojiajiri Watumishi wa nyumbani Walioajiriwa
Aina ya mkataba Mauzo Mkataba maalumu wa kazi Mkataba wa ajira
Kulipwa Baada ya kutoa huduma Kipindi cha kuzalisha bidhaa Kipindi cha kuzalisha bidhaa
Mkataba na Binafsi Mwajiri/mtu wa kati Mwajiri
Namna ya kuzalisha(inayotolewa na) kazini Binafsi Kujitegemea au kumtegemea mwajiri Mwajiri
Inayotolewa na Binafsi Binafsi Mwajiri
Usimamizi Hapana Usio wa moja kwa moja au haupo Usimamizi wa moja kwa moja
Uhuru wa kiuchumi Kamili Tegemezi Tegemezi

Soma zaidi

Fanya uchunguzi kuhusu sheria za kazi Tanzania. Na shiriki katika utafiti kuhusu mshahara, uweze kushinda zawadi!

loading...
Loading...