Kodi na Ushuru wa Biashara

Kodi, Ushuru, Forodha, Biashara, Tanzania, Kazi, Mishahara, Fedha, Wizara, Shirika, Nyongeza, Thamani, Ujuzi, VAT, Matumizi, Asilimia, Makampuni, Mapato, Ajira, Serikali, Mfanyakazi, Mwajiri, Sheria, Bidhaa

Kodi na Ushuru wa Biashara nchini Tanzania

Wizara ya Fedha inawajibika kubainisha muundo na uainishaji wa kodi. Kimsingi, kuna aina mbili za kodi zinazorejelewa kama kodi ya Moja kwa moja, ambayo kimsingi ni kodi ya mapato; il hali kodi Isiyo ya moja kwa moja ni kodi ya matumizi na biashara za kimataifa. Nakala hii itakufahamisha kuhusu baadhi ya kodi za kawaida ambazo watu wa biashara wanawajibika kulipia nchini Tanzania.

Je,  kodi ya Shirika ni nini?

Kama mwanabiashara utahitajika kulipa kodi ya Shirika Kodi ya mapato ya shirika ni kodi inayolipishwa kwa faida inayoweza kutozwa kodi ya shirika kwa makampuni yote yaliyosajiliwa na/au yanayofanya biashara Tanzania. Kiwando kinachotumika cha kodi ya mapato ya shirika ni asilimia 30, na kwa kawaida hulipwa katika hatua mbili. Kodi ya kwanza hulipwa kulingana na makadirio ya mlipa kodi mwenyewe mwanzo wa mwaka wa biashara; na kodi ya mwisho hulipwa baada ya utathmini rasmi wa mapato kamili mwisho wa mwaka wa mapato. Inalipwa katika Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA).

Je, Kodi ya Nyongeza ya Thamani (VAT) ni nini?

VAT ni kodi ya jumla ya matumizi kwenye nyongeza ya thamani ya bidhaa na huduma kwa kiwango cha kawaida cha asilimia kumi na nane (18%.) Ni kodi ya matumizi kwa sababu mwishowe inatoka kwa mtumiaji wa mwisho. Hailipishwi kwa makampuni. Inalipishwa asilimia ya bei, ambayo inamaanisha kwamba mzigo halisi wa kodi unaonekana kwa kila hatua ya uzalishaji na msururu wa usambazaji.

Je, Ushuru wa Kukuza Ujuzi ni nini?

Kodi nyingine ni Ushuru wa Kukuza Ujuzi, ambayo ni ushuru wa malipo, ambao unalipwa na waajiri wanaoajiri zaidi ya wafanyakazi wanne. Inatozwa kwa asilimia 6 ya mishahara. Kutoka kwa hii, asilimia 2 huenda moja kwa moja kwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa malengo ya kutoa ujuzi kwa wafanyakazi ambao waajiri wanahitaji. Ajira ya kilimo haiusishwi katika Ushuru wa Kukuza Ujuzi.

Je, Kodi ya zuio nini kwa ajira?

Kodi ya zuio, inayoitwa pia kama Kodi ya kukatalia, ni hitaji la serikali kwa mlipaji kwa kitu kinacholeta mapato ili kukatalia au kupunguza kodi kutoka kwa malipo, na alipe kodi hiyo kwa serikali. Nchini Tanzania, Kodi ya zuio hutumika sana kwa mapato ya ajira.
Mfano wa Kodi ya zuio ni kodi ya mshahara/mapato ya mfanyakazi (PAYE). Sehemu ya 81 ya Sheria ya Kodi ya Mapato inahitaji mwajiri kukatalia kodi kutoka kwa malipo yaliyolipwa mfanyakazi. Mwajiri anahitajika na Sehemu ya 84 (1) kulipia kodi iliyozuia kwa TRA kati ya siku saba baada ya mwisho wa kila mwezi wa kalenda.

Je, kuna kodi nyingine nchini Tanzania?

Tuna pia kodi ya biashara za kimataifa na zinajumuisha:

  • Ushuru wa Forodha
  • Ushuru wa Bidhaa
  • Kodi ya Nyongeza ya Thamani (VAT) kwenye Forodha
  • Kodi, ada, ushuru na gharama nyingine za mtumiaji za kindani, ambazo hukusanywa kutoka kwa vyanzo tofauti, kwa mfano kodi ya usajili wa Magari, kodi ya kuuza Magari, gharama ya huduma ya kuondoka bandarini na Angatua.

Kuna pia kodi nyingine ambazo hazijatajwa hapa na nyingine zinazohusiana na sekta/tasnia maalum, kwa mfano Kodi ya Mchezo wa Uwezonako na Kamari.

Soma zaidi

Ng’amua zaidi kuhusu Kazi na Mishara nchini Tanzania

loading...
Loading...