Tafauti ya kipato kijinsia

fahamu kuhusu tofauti ya kipato kijinsia, ni zipi sababu za tofauti ya kipato kijinsia na hali kimaifa iko vipi, yote katika Mywage Tanzania

Utofauti wa mshahara kijinsia

Utofauti wa mshahara kijinsia maana yake ni “tofauti kati ya wastani wa kipato anachopewa mtumishi wa kiume kwa saa dhidi ya kile anachopewa mtumishi wa kike kama asilimia ya jumla ya kipata anachopata mwanaume kwa saa”.

Utofauti huu hujitokeza pale ambapo mwanaume na mwanamke hulipwa kiwango tofauti cha pesa kwa kazi inayofanana au yenye thamani sawa. Utofauti wa ujira kijinsia unaofikia kati ya asilimia 17 na 22 maana yake watumishi wa kike hulipwa kidogo kwa saa kuliko wenzao wa kiume. Utofautin wa ujira kijinsia ndio kisababishi na madhara ya utofauti wa kijinsia.

Utofauti huu hujitokeza pale watu wanapolipwa kwa saa. Hivyo, ujira unapoandaliwa kwa wiki au kwa mwezi, huhesabiwa kwa saa pale panapowezekana.  
Kwa maana rahisi, utofauti wa ujira kijinsia ni nafasi/achano kati ya kipato cha mwanaume au mwanamke.

Nini sababu za utofauti wa mshahara kijinsia?

Utofauti wa mshahara kijinsia huweza kujitokeza kutokana na sababu nyingi ikiwemo:

•    Mienendo ya mtu binafsi: jinsia, umri, kiwango na aina ya elimu (kwa maana masomo uliyosoma), uzoefu kazini, ustahimilivu kazini, idadi ya watoto, ndoa,  mfumo wa maisha, rangi, na uhamaji, dini,
•    Mfumo wa kazi: kazi ya mkataba, muda wa kufanya kazi,(kazi za kufanya kwa saa dhidi ya zile za muda wote) na hali , taaluma, hadhi ya kazi husika,
•    Mienendo ya mwajiri/asasi husika: sekta ya uchumi, ukubwa au udogo wa kampuni, mshikamano uliopo.
•    Mgawanyiko: kwa mlalo au wima. Katika mgawanyiko wa mlalo, akina mama hurundikwa kwenye vijisekta vidogo/kazi zenye thamani na malipo duni. Katika mgawanyiko wima,  wanawake wachache ndio huajiriwa na kulipwa vizuri lakini bado hukabiliwa na vikwazo vingi katika kujiendeleza kitaaluma.
•    Kitaasisi: mafunzo ya kielimu na kiuweledi, makubaliano ya pamoja juu ya ujira, mahusiano ya kibiashara, sera zinazohusu likizo ya uzazi, matunzo ya mtoto,  kutunza wazee,
•    Maadili ya Jamii: elimu ya wanawake, uchaguzi wa kazi, aina ya kazi.

Nini wastani wa utofauti wa mshahara kijinsi duniani?

Wastani wa utofauti wa mshahara kijinsia duniani ni takribani asilimia 18, huku maeneo kama Ulaya, Oshenia, na  Latini Amerika, zikionesha  matokeo chanya kuliko Asia na Afrika ambapo upatikanaji wa taarifa au takwimu ni mgumu.
Asilimia hiyo inaweza kupimwa kulingana na taifa husika. Utafiti umeonesha tofauti ya mshara ya juu mpaka asimilia 46(Azerbaijan) katika taifa moja, na tofauti ya kiwango cha chini kabisa kwa asilimia 4 (Paraguay) kwa upande mwingine.

Kwa nini tofauti ya mshahara kijinsia ni muhimu?

Utofauti kati mshahara kijinsia huonesha jinsi kazi za wanawake zinavyothaminiwa. Huibua ubaguzi na mgawanyiko unaojitokeza katika mazingira ya kazi. Takwimu hizi huashiria:
Mkusanyiko wa wanawake katika kazi za muda mfupi, na katika kazi maalum.
•    Utofauti katika mgawanyo wa kazi za nyumbani ambapo akina mama huchukua sehemu kubwa ya majukumu.
•    Uwezekano mkubwa wa wanawake kuchukua likizo kutokana na kulea  watoto na familia.

Je, nini madhara ya utofauti wa mshahara kijinsia?

Utofauti wa mshahara kijinsia si tu kwamba unamwathiri mwa namke kiutendaji bali pia huathiri familia yake hasa pale anapokuwa ndiye anayetegemewa na familia kama mzazi mmoja. Utofauti huu wa kimshahara husababisha maisha duni, mlo hafifu, na hivyo kufanya utekelezaji wa malengo ya milenia ya kutokomeza umasikini na njaa kuwa ndoto.

Je, Shirika la Kazi Duniani (ILO) linasema nini kuhusu utofauti wa mshahara kijinsia?

Kanuni ya100 kuhusu mshahara sawa iliyopitishwa na ILO  mwaka 1951, huagiza kutoa mshahara unaolingana kwa wanaume na wanawake kwa kazi zenye thamani sawa. Ubaguzi wa kijinsia katika malipo, ni moja ya sababu ya utofauti wa mshahara kijinsia. Kanuni ya kutoa malipo sawa (Na. 100) ni moja ya kanuni nane kuu za ILO inataka kuaondoa ubaguzi katika malipo kwa kuhakikisha malipo sawa kwa wanaume na wanawake siyo tu kwa kazi zinazofanana lakini pia kazi zenye thamani sawa. Kanuni hii inaweza kutumika kupitia:

•    Sheria na taratibu za taifa;
•    Mamlaka zilizoanzishwa kisheria kusimamia na kupanga mshahara;
•    Makubaliano ya pamoja kati ya mwajiri na mwajiriwa; au
•    Mkusanyiko wa mbinu nyinine kama hizi.

Je, kanuni ya 100 ya ILO ya kutoa mshara sawa imeweza kuleta mchango chanya  kwenye utofauti wa mshahara kijinsia?

Utafiti umeonesha kuwa utekelezaji wa kanuni ya 100 ya ILO kutoa mshahara sawa inaweza kuwa na mchango chanya kwa taifa linaotoa mshahara tofauti kijinsia, na ushindani kiuchumi unaweza pia kuwa na mchango mkubwa.   
Hata hivyo, mara nyingi kanuni hizi ni sehemu ya mikakati inayotumiwa na serikali katika kuondoa utofauti uliopo katika jamii, kama vile kurahisisha uigiaji wa wanawake katika ajira kwa kuboresha huduma ya malezi kwa watoto, kuboresha upatikanaji wa elimu, na kuimarisha fursa ili kuwa maoni zaidi juu ya muda wa kufanya kazi.

Je, kujiunga na vyama vya wafanyakazi kunaweza kupunguza utofauti wa mshara kijinsia?

Utafiti juu mshahara unaonesha kuwa kunjiunga na vyama vya wafavyakazi kuna mchango mkubwa katika utofauti wa mshahara kijinsia, huku tofauti ikiwa ndogo katika mataifa ambako watumishi wamejiunga pamoja, kuliko yule mtumisha ambaye si mwanachama wa umoja wowote wa wafanyakazi. Hii inatokana na ukweli kuwa watumishi wakiwa pamoja mara nyingi hukubaliana kutoa mshahara sawa na masuala mengine kama hayo.

Je, elimu ya juu ina maana ya utofauti mdogo wa mshara kijinsia?

Utafiti unaonesha kwamba kuwa na elimuya juu kwa mwanamke siyo lazima kupelekee tofauti ndogo ya mshahara. Katika mazingira fulani, utofauti wa mshara huongezeka kadiri kiwango cha elimu kinavyoongezeka. Hata hivyo, kwa ujumla wake, elimu zaidi hupelekea mshara mkubwa.

Je, umri na kiwango cha huduma kinaathiri utofauti kati ya mshahara?

Ndio.Utafiti unaonesha kuwa utofauti wa mshahara huongezeka kadiri umri na miaka ya kutoa huduma inavyoongezeka. Kadiri mtu anavyokuwa mtu mzima, ndivyo mshahara unavyoongezeka. Vijana hulipwa kiasi kidogo kuliko watu wazima, kwa wastani. Watu wazima wa kiume hulipwa mshahara mkubwa sana kuliko ule wa wanawake vijana.

Je, kazi za kufanya kwa muda wote au zile za kufanya kwa saa zinaleta mabadiliko katika tofauti za mshahara kijinsia?

Ndio. Kwa sababu wanawake hubeba jukumu  kubwa la kulea na kufanya kazi za ndani, hii ina maana kuwa wanawake wengi wanafanya kazi kwa saa kuliko wanaume. Wanaume wanawasilishwa kwa kiwango kikubwa katika kazi zinazofanywa kwa saa, ambazo mshahara wake ni kidogo. Zaidi ya hayo, kazi saa hutoa fursa ndogo ya kupata cheo. Juu ya yote: wanawake wanaofanya kazi kwa saa hulipwa mshahara na mafao kwa saa!

Je, malezi ya mtoto yana athari gani kwa utofauti wa mshahara kijinsia?

Malezi ya mtoto yanaathari kubwa kwa wastani mshahara wa mwanamke. Katika baadhi nchi, wanawake hujiondoa kwenye soko la ajira pale wanapo olewa au kujifungua, na hivyo hurudi kazini baada kipindi fulani cha miaka. Mwanamke anaporudi kazini hulipwa kiasi kidogo ukilinganisha na mshahara aliokuwa akiripwa kabla ya kupumzika, na kupangwa kwenye kufanya kazi kwa saa au kazi ya kumwangamiza. Hali hii huitwa “Adhabu ya mtoto”.

Nchi chache zina utaratibu mzuri unaomruhusu wanamke kwenda likizo ndefu wanapojifungua na kulea watoto wao wachanga. Wanawake hawa wanaporudi kazini, huendelea na kazi zao za awali. Katika mataifa hayo, hakuna madhara yanayotokana na kulea mtoto kwenye suala la utofauti wa mshara kijinsia.

Je, utofauti wa mshahara hutokana na tathnia?
Ndio. Kisheria, ulinganifu katika mshahara kwa kazi zenye thamani sawa sharti uzingatiwe. Hata hivyo, kazi za kike kama vile kufanya usafi, elimu, afya, upishi, na uinjilisti, zina mshahara mdogo ukilinganisha na zile za wanaume. Hata hivyo, utofauti halisi katika mshahara unaweza kuonekana katika sekta ya fedha.

Je, bado kuna upendeleo kijinsia na kimshahara licha ya kuwepo kwa sheria?
Ndio. Upendeleo katika mazingira ya kazi upo, licha ya kuwepo kwa sheria. Kwanza, mshahara tofauti unatolewa kwa kazi zinazofanana, madhalani mwalimu wa kike na yule wa kiumewakiwa na sifa na uzoefu unaolingana hulipwa tofauti. Pili, upendeleo hujitokeza pale kazi tofauti, lakini zenye thamani sawa, zinakuwa na malipo tofauti. Katika hali hii, vigezo vinavyotakiwa katika kazi zinazofanywa na akina mama wengi kama vile ujuzi wa kuhudumia watu hupewa thamani ndogo kuliko zile za wanaume. Sehemu ya Kaskazini ya Ulaya upendeleo wa aina hii haupo hata kidogo.

Je, utofauti wa mshahara unaweza kuondolewa kuanzia ngazi ya chini, kitaifa na kimataifa?

Ndio – ILO inafanya. ITUC? inafanya. Utafiti unafanyika ili kukusanya takwimu. Angalia taarifa hapo ukurasa wa chini.

Je, mambo gani yanaweza kuboresha nafasi ya wanawake kazini, mbali na mshahara?

Zifuatazo ni sera zinazoweza kuleta ufumbuzi wa utofauti wa mshahara, na nafasi ya wanawake kazini:

•    Kuhimiza elimu.
•    Kuhimiza utunzaji wa mtoto – hii hurusu wanawake kuendelea kufanya kazi. Kucha kufanya kazi kwa muda mrefu, ina maana kuwa elimu zaidi inahitajika.
•    Hatua za kuhimiza elimu huwahamasisha wanawake kuchukua tathnia zinazofanywa na wanaume.
•    Sera zinazoruhusu ulinganifu katika mfumo wa maisha wa wazazi, kuhakikisha uzoefu wa wanawake na vyeo vyao kazini havitenguliwi.
•    Kuwepo utaratibu wa kutunza nafasi za kina mama kazini hata wanapo kuwa wamekwenda likizo ya uzazi. .
•    Kuajiri, kuchagua, na kupandisha vyeo ili kuhakikisha wanawake wanalibwa vizuri zaidi, na kazi zile zinazofanywa na wanaume.
•    Taratibu za kuungana, na makubaliano ya pamoja, hasa katika kazi zinazofanywa kina mama wengi mathalani, kazi za kufanya kwa saa, kwa muda mfupi, na zile za kufanyia nyumbani.

Njia kumi zinazoweza kumwezesha mwanamke kufunga utofauti wa mshahara kijinsia:

Jifunze mwenyewe.

•    Tafuta sekta ambapo unaweza kulipwa vizuri – kama vile chuma, uchimbaji wa madini, sekta ya kemia, nafasi ya uongozi serikalini au bungeni.
•    Fanya kazi siku nzima.
•    Nufaika na upandishaji vyeo wowote.
•    Nufaika na fursa yoyote ya kujiendeleza kielimu ukiwa kazini.
•    Fanya maafakiano juu ya malipo yako na kupanda kwa mshahara.
•    Change jobs now and then.
•    Komaa kikazi na endelea kuwajibika.
•    Fanya kazi na kampuni inayozingatia usawa katika kulipa mshahara na mambo   mengine kama hayo.
•    Tafuta kampuni kubwa kupita yote nchini na omba nafasi ya kazi.

loading...
Loading...